| |
| You are here : Mualiko wa Muhadhara na Futari ya Pamoja Ramadhan 2011 |
 |
| |
Mkutano wa dharura.
Kamati ya Maziko inafuraha kuwaalika nyote kuhudhuria mkutano wa dharura utakaofanyika
* Jumamosi Tarehe 03 december
* Kuanzia saa 14:00 mchana
* Pederlykkeskolen- Amager ( Brydesalle 25,2300 kbh.s)
Mada ya Mkutano huu ni kujadili kwa pamoja na kukubaliana mapendekezo ya marekebisho ya Katiba.Kutokana na muda ulivyokuwa mdogo,katika majadiliano yaliopita kuhusu hii katiba, kwenye mkutano wa mwaka uliofanyika kabla summer,
Kamati iliahidi kuitisha tena mkutano wa pamoja kwa ajili ya kumaliza suala la Katiba peke yake.
Kwa hivyo ni muhimu ndugu zetu wanaumoja kuhudhuria nyote,na kama mwanachama kushiriki katika kuendeleza umoja wetu kwa kuchangia fikra na maoni yako.
Kawaida mikutano kama hii ya dharura inakuwa gharama ya kufanya,kwa wakati unaotumika kwa kutayarisha, na matumizi yanayotoka kwa ajili ya vyakula na vinywaji (ambavyo vitaandaliwa bila malipo kwa wanaumoja).
|
|
|